Mwanamume akiwa amebeba miraa. [Picha/ farmerstrend.co.ke]
Mswada wa kupiga marufuku matumizi ya miraa katika Kaunti ya Mombasa unatarajiwa kuwasilishwa katika bunge la kaunti hiyo punde tu bunge hilo litakaporejelea vikao vyake.Mswada huo utawasilishwa bungeni na mwakilishi wadi Fatuma Swaleh.Swaleh alisema kuwa amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wanawake ambao waume wao ni waraibu wakuu wa miraa na muguka.Mwakilishi wadi huyo alisema kuwa wanawake hao wamelalamikia waume wao kukosa kuwatimizia haki zao za kimapenzi.“Nimepokea lalama nyingi kutoka kwa wanawake kwamba hawatimiziwi haki zao za kimapenzi, hivyo kunitaka niwasaidie kwa kuwasilisha mswada wa kupiga marufuku utumizi wa miraa na muguka,” alisema Fatuma.Swaleh amelitaja jambo hilo kama linalo changia wanawake wengi kuwa na ‘mipango ya kando’.“Wanawake wengi wanatafuta ‘mipango ya kando’ ili watimiziwe haki zao za kingono kwa sababu waume wao hawajiwezi na hawashughuliki wakati wa tendo hilo,” alisema Swaleh.Swaleh alisema kuwa vijana na wazee wengi Kaunti ya Mombasa wanatumia miraa na muguka, hali aliyosema imewasababisha kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6