Mitaa ya mabanda jijini Kisumu iinashuhudia uhaba wa vyoo, jambo ambalo linahatarisha maisha ya wenyeji.
Akizungungumza kwenye warsha ya usafi iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Umande Trust kuhusu namna ya kuimarisha usafi, Sheillah Simiyu, mwanafunzi katika chuo kikuu cha Stellenbosh Afrika kusini amesema kulingana na utafiti waliofanya, ni kuwa wakazi wengi katika mitaa ya mabanda hawana vyoo na vile vinavyopatikana katika maeneo hayo ni chafu.
Utafiti huo umebaini kuwa vyoo vingi katika mitaa ya mabanda huporomoka kunapotokea mvua kubwa.
Simiyu amedokeza ni vyema kwa wamiliki wa makaazi kushirikiana kwa pamoja na serikali ya kaunti ya Kisumu katika kuimarisha usafi kwenye mitaa ya mabanda.
Halkadhalika, makazi hayo ya mabanda yamesajili visa vikubwa vya magonjwa yanayoambukizwa kutoka na mazingira machafu, jambo ambalo amesema limekua donda sugu kwa mda mrefu sasa.
Ameihimiza serikali ya Kisumu vile vile kuhimarisha viwango vya afya katka mengi ya makaazi hayo.