Mtalii mmoja kutoka Ujerumani amehukumiwa mwaka mmoja jela kwa kosa la kuwa humu nchini kinyume cha sheria.
Birtel Markus alitiwa mbaroni siku ya Jumatatu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi, akiwa na stakabadhi zinazoonyesha muda wake wa kuwa humu nchini ulikamilika Agosti 11, mwaka huu.
Markus alikubali mashtaka hayo mbele ya Hakimu Martin Rabera.
Wakili wake Vincent Mogaka alisema kuwa mshtakiwa huyo alikuja nchini kama mtalii na kupoteza cheti chake cha usafiri, hatua aliyoitaja kumfanya kurudi kwao.
Hakimu Rabera alimhukumu mwaka mmoja jela ama kuachiliwa kwa faini ya shilingi laki moja.