Mtalii wa Marekani amefikishwa katika mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kumiliki bunduki bila kibali.
Mahakama ilielezwa siku ya Jumatatu kuwa mshtakiwa, Richardson Rollier, pamoja na mchumba wake raia wa Kenya Mercy Mwendwa, wanadaiwa kupatikana na bunduki kinyume cha sheria katika makaazi yao huko Nyali, mnamo Machi 19, 2016.
Wawili hao walikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Mkuu Susan Shitub.
Hakimu Shitub aliwaachilia kwa dhamana ya shilingi 500,000.
Kesi hiyo itasikilizwa Mei 26, 2016.