Mbunge wa Malindi Willy Mtengo amelalamikia ukosefu wa maji safi ya kunywa katika eneo bunge lake na katika Kaunti ya Kilifi kwa jumla licha ya kaunti hiyo kuzalisha maji safi kutoka Baricho.
Akizungumza wakati wa kongomano la washikadau katika sekta ya maji lilofanyika katika mkahawa wa Pride Inn jijini Mombasa, Mtengo alisema kuwa ukosefu waji katika eneo hilo limekuwa donda sugu.
Aidha, Mtengo alisema kuwa eneo bunge hilo lina miradi ya maji ambayo haijakamilishwa kwa miaka mingi, na kuitaka serikali ya kaunti na ile ya kitaifa kuingilia kati na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa.
Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri wa Maji nchini Eugine Wamalwa alitoa makataa ya siku 21 kwa bodi ya maji katika kanda ya Pwani kuanza miradi ya usambazaji maji safi katika eneo la Malindi, ambalo limekuwa likikumbwa na changamoto ya uhaba wa maji mara kwa mara.