Mtoto wa umri wa miaka tatu unusu aliaga dunia hapo siku ya Jumamosi baada ya kutumbukia bwawani moja katika eneo la Uvaini, kata ndogo ya Makutano katika kaunti ndogo ya Yatta.
Kwa mujibu wa naibu wa chifu wa kata ndogo ya Makutano Esther Nthenya, mtoto huyo aliondoka nyumbani na watoto wenzake na kwenda kucheza kando ya bwawa hili kabla ya yeye kutumbukia na kuaga dunia.
Nthenya alipendekeza mabwawa pamoja na visima vilivyo karibu na boma za watu kuwekewa ua ili kuzuia ajali za aina hii.
Vilevile chifu huyo aliwataka wazazi walio na watoto wachanga kuwa waangalifu mno na kujua watoto wao waliko ili kuepuka visa kama hivi.
Mwili wa mtoto huyo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Matuu Median katika mji wa Matuu