Wakaazi wa Timboni eneo la Mvita leo waliamkia asubuhi ya tarehe 29 Juni kupatana na mwili wa mtoto mchanga aliyetupwa eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwa mujibu wa Pilipili FM, kisa hicho kilichotokea asubuhi kiliwaacha wakaazi na mshtuko huku wakiwa na ghadhabu kwa msichana aliyetenda kitendo hicho cha unyama. 

"Twawasihi vijana wote wa kike na kiume kuwa makini na kuyaelewa majukumu yao ya kimaisha. Hii ni pamoja na kuwalea watoto wanapopata mimba la sivyo wajiingize kwenye mpango wa kupanga uzazi," wakaazi waliteta.

Wakaazi hao wamesema mara nyingi eneo hilo la Timboni limekuwa ndilo ghala la kuwatupa watoto, jambo ambalo wanalitaka likome mara moja. 

"Twatoa wito kwa polisi kukichungiza kisa hiki kipotovu na kumchukulia mhusika hatua za kisheria," wakaazi walisema.