Mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka mitano unusu, anauguza kwenye hospitali kuu ya Bahati, baada ya kudhulumiwa kimapenzi Jumatano jioni katika eneo la Satellite, wadi ya Bahati kaunti ya Nakuru.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mamake mtoto huyo Ann Ekai alisema kwamba walikuwa wanaenda kuteka maji, ambapo mtoto wake alimtangulia, lakini alipofika mahala pale hakumpata mtoto.

Alipoteka maji na kurudi nyumbani, alimpata mtoto akiwa amelala nyuma ya nyumba, bila mavazi.

“Nilimpata amelala kifudifudi, hana suruali, na nilipomwambia aamke nikaona anashindwa hata kutembea,” Ekai alisema.

Hapo ndipo mtoto alimwelezea kuwa, kijana mmoja ambaye inasemekana ni kijakazi wa shamba la nduguye, alimshika na kumlawiti.

“Nilipomuuliza nini kinamfanya atembee hivyo, aliniambia kwamba kijana anayefanya kazi kwa nduguye mkubwa alimtendea tabia mbaya,” Ekai alisema.

Kulingana na mtoto huyo, mshukiwa ambaye sasa anatafutwa na polisi, alimtendea unyama huo kwenye jumba moja ambalo halijakamilika kujengwa, huku akimtishia kutomwambia yeyote.

Wazazi wake walimpeleka mtoto huyo hospitalini, ambapo anaendelea kupata matibabu, na badaye kuripoti katika kituo cha polisi cha Bahati eneo la Maili Kumi.

OCPD wa Nakuru Kaskazini Duncan Nguthu amedhibitisha kisa hicho.