Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Rangenyo baada ya mtoto wa umri wa miaka mitatu kuaga dunia kwenye eneo la uwakilishi wadi ya Nyamaiya baada ya kuangukiwa na mchanga kwenye timbo la mawe mapema Jumamosi. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akithibitisha kisa hicho, chifu wa kata ya Mugirango magharibi Dancan Moriasi alisema tukio hilo limewaacha wazazi wa mwendazake na majeraha makali huenda limesababishwa na mvua nyingi inayoendelea kunyesha katika eneo hilo. 

"Tukio hilo limewaacha wazazi wa mwendazake na majeraha makali na tunashuku kwamba huenda ajali hiyo ilisababishwa na mvua nyingi inayoendelea kunyesha," alisema Moriasi. 

Moriasi aidha aliwatahadharisha wakazi wa eneo hilo kujiepusha na uchimbaji mawe kwenye msimu wa mvua. 

"Mvua nyingi inaendelea kunyesha na ni hatari sana kwa wananchi kuendelea kuchimba mawe na kupasua kokoto, na ni himizo langu kwao kuepukana na timbo hizo hadi msimu wa kiangazi," aliongezea Moriasi. 

Mwili wa mwendazake umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Nyamira huku majeruhi wakiendelea kupokea matibabu kwenye hospitali hiyo.