Mtu mmoja ameaga dunia mapema Jumanne huku wengine wawili wakipata majeraha mabaya kufuatia mkasa wa ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi kueleka Nakuru.

Share news tips with us here at Hivisasa

Watatu hao walikuwa wakitoka kwenye shughuli ya mazishi huko Gilgil wakati waligongwa na lori moja eneo la Marula yapata kilomita tano kutoka mji wa Naivasha.

Mmoja wa walioshuhudia James Kuria amesema kuwa watatu hao walikuwa wakielekea mjini Naivasha wakati walikumana na mauti hayo, huku walioapata majeraha wakikimbizwa katika hospitali kuu ya wilaya ya Naivasha wakiwa katika hali mahututi.

"Waathiriwa walikuwa wakija hapa Naivasha lakini hawakuweza kufika baada ya ajali yenyewe na walikuwa hali mahututi," alisema Kuria.

Afisaa mmoja wa ngazi ya juu wa polisi ambaye hakutaka kutajwa jina lake amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa wamesikitishwa na idadi kubwa ya ajali zinazowalenga waendeshaji wa pikipiki maarufu kama boda boda.