Jamaa mmoja mwenye umri wa makamo ameaga dunia Alhamisi hii Usiku baada ya kunywa pombe haramu aina ya chang’aa katika kijiji cha hodihodi kilicho Kabatini kwenye eneno la Bahati katika kaunti ya Nakuru.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwili wa marehemu mwenye umri wa miaka 23 ulipatikana na wapita njia Ijumaa hii asubuhi mwndo wa saa kumi na mbili asubuhi na kupelekwa katika ufuo wa kaunti ya Nakuru.

Ni hatua iliyopelekea wakaazi wa eneo hilo kufanya maandamano hadi katika makao makuu ya polisi ya divisheni ya Bahati wakitaka maafisa wote katika kituo hicho wapewe uhamisho.

Baadhi wao waliwashutumu maafisa hao kwa kufeli kukabiliana na uuzaji wa Pombe haramu katika eneo hilo badala ya kuwanyanyasa waendeshaji wa pikipiki katika eneo hilo.

Hata hivyo, mwakilishi wa wadi ya Kabatini Paul Thuo Mwangi alituliza hali hiyo baada ya kuzungumza na uma.

Kwa upande wake Mbunge wa eneo hilola Bahati Kimani Ngunjiri kupitia kwa njia ya simu amesema amezungumza na inspekta Generali wa polisi Joseoh Boinnett mara kwa mara akitaka OCPD wa Baharti Duncan Nguthu apewe uhamisho bila mafanikio.

Amesisitiza kuwa chifu wa MAILI Sba pia anafaa kufutwa kazi kwa kila anachodai kama hatua yake ya kukosa kukomesha Pombe haramu katika eneo hilo.

Hata hivyo, amesema atamrai katibu wa kudumu katika wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho kukabiliana na maafisa hao wawili kwa muujibu wa sheria.