Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mtu mmoja amekimbizwa katika hospitali kuu ya mkoa ya bonde la ufa iliyo hapa mjini nakuru, huku mali yenye dhamani isiyojulikana ikiteketea karibu soko la Top Market Nakuru.

Hayo ni baada ya Moto kuzuka siku ya Jumatano kwenye hoteli moja ndogo iliyo karibu na soko hilo.

Inaarifiwa moto huo ulisababishwa na hitilafu za umeme zilizosababisha mafuta yaliyokuwa yakikaanga vibanzi au chips kushika moto.

Moto huo ulisambaa na kuteketeza vibanda vingine vitatu ikiwemo cha kuuza nguo.

Zima moto kutoka kaunti ya Nakuru hata hivyo walifika eneo la tukio na kuzima moto huo baada ya wafanyakazi wa kampuni ya umeme kuzima umeme huo.