Mtu mmoja amedhibitishwa na kufariki huku wengine wakitibiwa kwenye hospitali ya Naivasha baada ya mzozo kwenye shamba la ADC Naivasha kutibuka.
Mzozo huo ulitibuka Jumapili huku jamii mbili kwenye eneo hilo zikikabiliana vikali na mtu mmoja kuuawa.
“Tayari mtu mmoja amefariki na wengine kupelekwa kwenye hospitali,” Ole Kiseri alisema Jumapili jioni.
Aidha umiliki wa shamba hilo ndio ulileta mzozo huo.
OCPD wa Naivasha Titus Munyoki allidhibitisha kisa hicho.
Munyoki alisema hali imedhibitiwa baada ya maafisa wake kufika eneo hilo.
Hata hivyo, Hillary Oleparsiene alisema hofu ingali imetanda huku baadhi ya wakazi wakihama kwa kuhofia kisa cha kulipiza kisasi.