Mwenyekiti wa wabunge wa Pwani Gideon Mung'aro amepokonywa wadhfa huo na kupewa Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga baada ya kufanyika kura ya uchaguzi wa viongozi wa muungano wa wabunge wa Pwani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mung'aro aliyepia mbunge wa Kilifi Kaskazini amebaduliwa kwa wadhfa huo baada ya wabunge 17 kati ya 39 kumchagua Gunga Mwinga kuwa mwenyekiti wa wabunge huo katika uchguzi uliyofanyika siku ya Jumatano katika eneo la Pwani.

Wafuasi wanaomuunga mkono Mung'aro wakiongozwa na mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kilifi Zainab Chidzuga kudai kuwa uchaguzi huo ulipangwa na baadhi ya watu fulani kwa kuwahonga wabunge hao kumbandua Mung'aro kama mwenyekiti wa wabunge wa Pwani.

"Kuna udanganyifu na uhongaji fulani umefanywa na baadhi ya viongozi ili kumbandua Mung'aro katika wadhfa huo kwani sisi hatuoni sababu za kiongozi mchapa kazi kukosa kuchaguliwa na kumchagua kiongozi ambaye hawezi kuwaunganisha viongozi wa Pwani, mimi sio kama uchaguzi huu umekuwa sawa," alisema Chidzuga baada ya matokeo ya uchaguzi huo siku ya Jumatano.

Wanaomuunga mkono Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwingi wamepongeza uchaguzi huo na kusema kuwa Gunga atafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa viongozi wa Pwani wanaungana na kuleta mabadiliko makubwa kwa Wapwani sambamba na kubuni chama kimoja kitakacho waunganisha viongozi wa Pwani.

Uchanguzi huo wa Mwenyekiti wa wabunge wa Pwani umejiri wiki moja tu baada ya kufanyika uchaguzi mdogo wa Malindi siku ya Jumatatu na Willy Mtengo wa chama cha ODM akanyakua ushindi huo na kuwa mbunge wa Malindi.