Wanasiasa katika kaunti ya Kisii wameombwa kutoingiza siasa katika ukarabati wa uwanja wa michezo katika eneo la Nyaturago eneo bunge la Nyaribari Chache kaunti ya Kisii.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hii ni baada ya baadhi ya wanasiasa kuiandikia barua serikali ya kitaifa ili isimamishe ukarabati huo mwaka jana wakidai kuwa ukarabati huo hukuwa miongoni mwa miradi ya maendeleo katika eneo bunge hilo.

Richard Tong’i aliomba wanasiasa kutoingiza siasa kwa ukarabati huo wa uwanja huku akisema hiyo ni njia moja ya kuwapa vijana fursa ya kupata kazi, kuinua vipaji vyao na kuinua uchumi wa kaunti miongoni mwa mengine mengi.

“Uwanja huu wa Nyaturago ungejengwa mwaka jana lakini baadhi ya wanasiasa wakaandikia serikali barua ya kusimamisha ukarabati huo," alisema Tong'i.

"Kwa kile walichodai ni kutokuwa miongoni mwa miradi ya maendeleo lakini mwaka huu tumepata pesa na utajengwa rasmi na hayo ni maendeleo,” aliongeza Tong’i.