Changamoto imetolewa kwa viongozi wa upinzani kutoendeleza siasa tu za kupinga kila jambo bali washiriki katika siasa za kuleta maendeleo.
Akizungumza na wakazi wa Mombasa wakati wa kufungua afisi ya Maendeleo Chap Chap katika eneo bunge la Changamwe kaunti ya Mombasa, Gavana wa Machakos Alfred Mutua amesema kuwa upinzani umejaa viongozi walio mahiri na wanaojulikana kote ulimwenguni hvyo ni sharti walete mired ya maendeleo kama vile barabara ,kutafuta masoko ya kuuza bidhaa mbali mbali ili waweze kuchangia katika maendeleo ya taifa hili.
Kulingana na Mutua mtu yeyote anayetaka kupigiwa kura na wananchi ni sharti atekeleze wajibu wake kwa kutumikia wananchi.
Wakati huo huo Mutua amesisitiza kuwa atasalia katika chama cha Wiper hadi pale atakapofukuzwa na iwapo hilo litafanyika atapata chama mbadala.