Mwenyekiti wa NACADA John Mututho amekemea tukio la kuzomewa kwa gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua wakati wa ziara ya rais Kenyatta.
Mututho alisema hakuna haja ya viongozi kuaibishana wakati kuna wageni wa haiba ya juu kama rais kwa sababu ya siasa.
Mututho alisema wakati wa siasa za 2017 utafika na gavana Mbugua kubanduliwa iwapo hajafanya kazi ipasavyo.
“Mimi nataka nikashifu kisa cha gavana Mbugua kuzomewa na wananchi. Huenda hilo lilipangwa na watu fulani na ni vibaya,” Mututho alisema.
Mututho alisema Kinuthia anafaa kuheshimiwa kwa sasa kwani yeye ndiye gavana kwa wakati huu.
“Ni vyema tuheshimuKinuthia kwani kwa sasa ndiye gavana,” Mututho alisema.