Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga katika hafla ya awali. Picha/ citizentv.co.ke
Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga ameushutumu muungano wa jumuia ya kaunti za Pwani kwa kile alichokitaja kama kushindwa kuleta maendeleo na umoja kwa wakaazi.
Akizungumza na wanahabari katika eneo bunge lake siku ya Jumatatu, Gunga alisema kwamba tangu kubuniwa kwa muungano huo, bado hakujashuhudiwa mabadiliko yoyote katika kaunti zote sita za ukanda wa Pwani.Mbunge huyo alisema kuwa kaunti hizo bado zinaendelea kupitia changamoto nyingi za kimaendeleo.Mwinga aidha alisema kwamba kuna haja ya viongozi wa Pwani kujitenga na tofauti zao za vyama vya siasa, kwa kuwa hatua hiyo ndiyo imechangia kuzorota kwa muungano huo.“Endapo muungano huu utakumbatiwa vizuri, basi huenda ukainua viwango vya uchumi na maendeleo katika eneo la Pwani,” alisema Mwinga.