Muungano wa Wabunge wa Pwani ulifanya uchaguzi jijini Nairobi siku ya Jumatano.
Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga wa chama cha KADU-Asili ndiye aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa muungano huo, huku mwakilishi wa wanawake wa Lamu Shakila Abdallah wa chama cha Wiper akichaguliwa kuwa naibu wake.
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir alichaguliwa kushikilia wadhifa wa uratibu katika muungano huo wa wabunge wa Pwani.
Muungano huo pia ulimchagua mbunge wa Voi Jone Mlolwa kuwa katibu mkuu, huku kiranja akiwa Aisha Jumwa, na mweka hazina Zulekha Hassan.
Muungano huo utakuwa ukishauriwa na Hassan Mwanyoya na mbunge wa Wundanyi Thomas Mwadeghu.
Hapo awali, muungano huo ulikuwa ukiongozwa na mbunge wa Kilifi Kazkazini Gideon Mungaro.
Wabunge 19 wa Pwani ndio waliohudhuria hafla hiyo.