Muungano wa walimu wakuu nchini KSSPA, umeandaa mkutano wa kujadili changamoto zinazokumba shule za upili na hasaa swala la wizi wa mitihani wa kitaifa ambalo limekua donda sugu.
Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatano, mkuu wa muungano huo John Awiti, alisema kuwa kama walimu wanaunga mkono mabadiliko yaliyofanywa na wizara ya elimu katika kalenda ya mfumo mpya wa elimu.
Hata hivyo, Awiti alilalamikia changamoto ambazo walimu wakuu hupitia shuleni.
“Walimu wakuu wanafaa kupewa muda wa kupumzika kwa kuwa zaidi ya walimu wakuu 23 hufa kila mwaka kwa kuzidiwa na msongo wa mawazo na kazi nyingi,” alisema Awiti.