Muungano wa wanaougua maradhi ya kifafa eneo la Pwani Kawe umesema takriban watu milioni moja nchini wanaugua ugonjwa wa kifafa lakini kati yao ni laki mbili tu wanapata matibabu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Katika mkutano uliofanyika katika shule ya msingi ya Mvita siku ya Jumatano, mkurugenzi wa muungano huo Stephene Kimwaki amesema ni asilimia arubaini tu ya wagonjwa hao wanaopata matibabu kwa sababu wengi wanaamini kifafa ni ugonjwa wa kurogwa ama kurithi na hauna tiba.

Ameeleza kwamba ugonjwa huo ni sawa na maradhi mengine yanayotibika na huletwa na hitilafu kwa ubongo.

Katika mkutano huo wa kuadhimisha siku ya watu walio na maradhi ya kifafa, mwaathiriwa wa ugonjwa huo Naima Omar amemsimulia mwanahabari wetu yanayomkumba kutokana na ugonjwa huo.

Amesema changamoto anayopitia ni kukimbiwa na kunyimwa fursa ya kufanya kazi nyengine nyumbani kwa kudaiwa hawezi sababu ya ugonjwa huo licha ya kujiamini kuchukulia ugonjwa huo kama magonjwa mengine.