Muungano wa watengezaji viatu maarufu Kenya Footwear Manufacturers Association umeundwa katika kaunti ya Nakuru. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hafla hio ya Ijumaa ilishuhudiwa na afisa mkuu wa Kenya Leather Development Council KLCD Charles Mwangi Kinyanjui ambaye alihimiza washikadau kuchukulia kwa uzito sekta hiyo ya bidhaa za ngozi humu nchini. 

"Sababu kuu ya sekta hii kusalia nyuma no kutokana na hatua ya washikadau kutengeza bidhaa ambazo haziwezi kutosheleza soko," alisema Kinyanjui ambaye amekuwa katika sekta hiyo Kwa zaidi ya miaka 30. 

Wakati wa hafla hiyo poa viongozi wa Kenya Footwear Manufacturers Association tawi la Nakuru walichaguliwa. 

Beatrice Mado ndiye mwenyekiti, Nathan Omollo katibu ilhali Vinicent Kikaya ndiye mweka hazina. Watatu hao waliapa kushirikiana katika kuinua sekta ya kutengeza viatu kutokana na ngozi. 

Baadhi ya washikadau katika sekta ya kutengeza viatu Nakuru.