Muungano wa wauguzi umetoa ilani ya mgomo kuanzia Juni tarehe mosi iwapo matakwa yao hayatazingatiwa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na habari kutoka kwa katibu mkuu wa muungano huo, Seth Panyako, mgomo huo utakuwa wa taifa zima. Katibu mkuu huyo amesisitiza kuwa wauguzi wameendelea kufanya kazi katika hali ngumu bila maslahi yao kuangaziwa na serikali kuu na ile ya kaunti.

Aidha, katika kaunti zingine wauguzi wamekuwa wakigoma huku wakiteta kuwa mazingira yao ya kikazi hayajazingatiwa na mishahara yao ni duni ikilinganizwa na kazi wanayoifanya katika hospitali za kaunti mbalimbali nchini.

Iwapo mgomo huo utakuwa, wagonjwa wengi hawatapata huduma katika hospitali za umma ila watatafuta uzaidizi wa kimatibabu katika hospitali za kibinafsi ambazo kwa mara nyingi ulipisha pesa nyingi ikilinganishwa na zile za umma.