Muungano wa wasomi wa Naivasha unataka bodi ya kaunti ya iliyobuniwa ili kutoa leseni kwa vilabu kuchunguzwa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Haya yamejiri wiki moja tu baada ya bodi hiyo kufutilia mbali leseni kwa asilimia hamsini za vilabu vyote mjini Naivasha.

Mkurugenzi mkuu wa muungano huo Absolomon Mukhusi alisema kuwa wataelekea mahakamani ili kupinga hatua iliyochukuliwa na bodi hiyo.

Akizungumza na wanahabari mapema jumatatu mjini humo, Mukhusi alisema kuwa wanachama wa bodi hiyo wanawahangaisha wamiliki wa vilabu na kudai kuwa wanaitisha hongo ili kutoa leseni hizo.

"Ikiwa bodi hii imeundwa tu majuzi na inaanza kuhangaisha wenye vilabu, bodi yenyewe inaokena ina kasoro! Hawafuati utaratibu wa kuangalia uhalali wa leseni hizi za mivinyo, wanafaa kufanya kazi yao kwa ustaarabu," alisema Bw Mukhusi.

Hata hivyo mmoja wa wanachama wa bodi hiyo Charles Mburu amekana madai hayo na kusema kuwa hayana msingi wowote.