Makundi ya wanawake katika eneo la Mvita yametajwa kuwa miongoni mwa makundi bora katika eneo la Pwani, yanayolipa mikopo yao kwa wakat ufaao.
Daniel Waheka, ambaye ni mshirikishi wa hazina ya kitaifa ya Wanawake, amedokeza kuwa makundi katika eneo bunge la Mvita yanalipa fedha hizo za mikopo kwa wakati ufaao ikilinganishwa na makundi mengine Pwani.
Akizungumza katika uwanja wa Tononoka, wakati wa kukabidhi hundi kwa makundi hayo, Waheka alisema kuwa fedha hizo zitawasaidia kinamama kuboresha shughuli zao za kimaendeleo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir aliseme kuwa wataanzisha mikakati kwa ushirikiano na hazina hiyo kuwahamasisha vijana kujiunga na makundi ili kunufaika na mikopo hiyo.
Nassir alisema kuwa kupitia mikopo hiyo, vijana wanaweza kujihusisha katika miradi ya kuwanufaisha.