Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanyabiashara wengi katika soko kuu la Kongowea wamelazimika kufungua biashara zao kuchelewa kutokana na mvua iliyokua ikinyesha.

Wakizunguza na mwanahabari huyu siku ya Alhamisi, wafanyabiashara hao wamedokeza kuwa kutokana na kuwa maeneo mengi ya soko hilo ni maeneo ya wazi, wanalazimika kusubiri hadi mvua inapoisha ili kufungua biashara zao.

Mwanahamisi Juma, mmoja wa wafanyibiashara hao alisema kuwa ni vigumu kufuata bidhaa kwenye magari wakati wa mvua.

Wakati huo huo, wanabishara hao walisema kuwa iwapo mvua hiyo itaendelea kupita kiasi itaathiri pakubwa shughuli za kibiashara sokoni humo, na kusababisha hasara kati mwao ikizingatiwa kuwa wengi uuza katika sehemu wazi za soko hilo.

“Biashara itapungua iwapo mvua itaendelea kunyesha kwa sababu wateja watapungua, na hapa kwa mvua hatuwezi fanya biashara,” alisema Mwanahamisi.