Shughuli zimesitishwa Kwa muda Jumanne jioni hii ni baada ya mvua kubwa kusababisha mtafaruko mtaani Manyani.
Mvua hiyo iliyoanza majira ya saa kumi na moja jioni ilipelekea mitaro mtaani humo kupasuka na kupelekea maji kutapakaa barabarani.
Ni hali iliyofanya wakaazi kama vile wa mtaa wa Manyani kungojea hadi pale maji hayo kupungua.
Hata hivyo, baadhi ya wahudumu wa pikipiki waliozungumza na mwanahabari huyu walilaumu uongozi wa kaunti Kwa kujenga mitaro midogo ambayo hulemewa na mvua. Walitoa wito kwa serikali kukarabati mitaro hiyo na kuipanua la sivyo hali hiyo itaendelea kushuhudiwa.