Sehemu ya barabara ya Nakuru magharibi iliharibiwa na mvua iliyonyesha mjini Nakuru siku ya Ijumaa na kutatiza shughuli za usafiri katika barabara hiyo.
Wenye magari walipata balaa kuelekea eneo hilo kutokana na hali iliyokadiriwa na mvua nyingi huku wakiomba usaidizi kutoka kwa serikali ya kaunti.
"Baada ya hii mvua, sehemu kadhaa zimeharibika na imekua vigumu kwetu kuelekea upande mwingine, tumeteseka sana hii leo," alisema Franklin Njuguna.
"Tunaiomba serikali ya kaunti ifanye marekebisho katika barabara hii maana mvua ikiendelea, hali itakuwa mbaya zaidi.