Mvua kubwa ambayo ilinyesha katika eneo la Rongai Jumatatu jioni, iilisababisha mafuriko yaliyofunga barabara ya Kwa Gitau kuelekea Ol-Rongai Centre kwa muda wa saa tatu, huku wanafunzi na wakaazi wakilazimika kusubiri pembezoni mwa barabara ili maji yapungue.
Kando na kusababisha mafuriko, upepo mkali uliokuwa umeandamana nayo ulingoa paa za maduka manne katika kituo cha kibiashara cha Kwa Gitau.
Kulingana na wakaazi waiozungumza na mwandishi huyu katika eneo hilo, mvua hiyo pia iling’oa miti kadhaa huku madereva wa magari ya umma ya kutoka na kuingia Ol-rongai, wakilazimika kutafuta njia mbadala ya kurejea kwenye barabara kuu ya Nakuru Eldamaravine, na hatimaye Nakuru mjini.
Mkaazi willaim rono alisema: “Mvua hii imekuwa ni ya ajabu kwa sababu kwa miaka kadhaa hatujaona mafuriko hapa. Watu wanavukishwa kwa mikokoteni haswa wanafunzi wa shule. Stima imepotea eneo hili lote, na huenda leo tukalala kwenye giza.”
Kati ya waliotatizika ni watoto wa shule ya msingi ya Olrongai, shule ya upili ya Ol-rongai pamoja na Chief Kariuki Academy ambayo ni ya kibinafsi..
Magari ya kibinafsi na piki piki pia hayakusazwa pia na mvua hiyo ya lisaa limoja tu.