Mvulana wa miaka ya kumi na nane aliaga dunia hapo siku ya Jumatatu alipokuwa akiogolea katika bwawa la Masinga katika eneo la Kathukini kaunti ndogo ya Masinga.
Kwa mujibu wa naibu wa chifu wa Kata ndogo ya Kathukini Julius Katoni alisema kuwa mvulana huyo alikuwa ameandamana na vijana wawili kuenda kuogolea kabla ya janga hilo kutokea.
Aidha, Katoni alielezea kuwa mvulana huyo alijitosa majini na kuzama pale alingojewa aibuke bila mafanikio.
Kulingana na Katoni watu wenye ufundi wa kuogelea walijitosa majini kumwokoa kijana huyo baada ya wenzake kupiga mayowe lakini alipatikana amekwama kwenye mizizi ya miti akiwa mfu.
Chifu huyo aliwataka wenyeji kuwa waangalifu wanapoogelea kwani visa vya watu kufa maji vimekuwa vikishuhudiwa.
Polisi waliuchukua mwili na kupeleka katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Matuu median.