Mvulana mwenye umri wa miaka 22 amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kumnajisi na kumpachika mimba msichana wa miaka 16.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mshatkiwa, Saidi Khamisi, anadaiwa kutekeleza kitendo hicho siku tofauti kati ya mwezi Septemba mwaka jana na mwezi Aprili mwaka huu, katika eneo la Likoni.

Mahakama ilielezwa kuwa ripoti kutoka kwa hospitali inaonyesha kuwa msichana huyo ana ujauzito wa miezi miwili.

Bwana Said alikanusha mashtaka hayo siku ya Ijumaa mbele ya hakimu mkuu Teresia Matheka.

Hakimu Matheka aliagiza mshtakiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja unusu.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe Juni 9 mwaka huu.