Naibu mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Salim Mvurya ameihimiza serikali kuzingatia ugatuzi na kutenga fedha za kutosha katika serikali za ugatuzi nchini ili kuhakikisha kuwa maswala yanayowalenga Wakenya mashinani yanatekelezwa.
Mvurya ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Kwale amehimiza sekta zote za umma kugatuliwa ili kuhakikisha kuwa miradi kutoka kwa sekta hizo zinaingilia na serikali za ugatuzi.
Mvurya amesema kuwa Kongamano hilo la tatu la magavana lilioandaliwa mjini Meru limepitisha maswala 18 za kufanikisha ugatuzi mashinani kwa lengo la kuboresha miradi mbalimbali itakayowafaidi Wakenya.
Amesema kuwa maswala hayo ni pamoja na kuimarisha sekta ya afya, maji na usalama huku viongozi wa serikali za ugatuzi wakishikilia kupiga vita ufisadi nchini ili kuwanufaisha Wakenya kutokana na raslimali zao.
“Tumemaliza kongamano letu njema na maswala ambayo tumeyapitisha tutahakikisha yanamfaidi mwananchi mashinani ili kufanikisha ugautuzi,” alisema Mvurya mjini Mombasa siku ya Jumamosi wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu ugatuzi.