Gavana wa Kwale Salim Mvurya katika hafla ya awali. Amewakashifu viongozi wa upinzani kwa kuongelea siasa katika mazishi ya Senator Boy. Picha/standardmedia.co.ke
Gavana wa Kwale Salim Mvurya amemkashifu kinara wa Cord Raila Odinga kwa kuzungumza mambo ya siasa katika mazishi ya Seneta wa Kwale Boy Juma Boy.
Mvurya amekosoa hatua hiyo na kulitaja kama jambo lisilokua la msingi, ikizingatiwa ilikuwa siku ya huzuni kwa wakaazi wa Kwale.“Sio vizuri kuongelea siasa wakati wa mazishi kwani siasa ina muda wake,” alisema Mvurya.Gavana huyo amewataka viongozi kutozungumzia siasa wakati wa hafla mbalimbali za jamii kama vile mazishi.Aidha, Mvurya amewakashifu viongozi wa upinzani kwa kile alichokitaja kama kuchochea na kujaribu kugawanya wananchi wakati wa mazishi.
“Tuepukeni kutenganisha wananchi kwa misingi ya siasa wakati wa mazishi,” alisema Mvurya.
Kauli yake inajiri baada ya wanasiasa wa Cord kuongelea siasa wakati wa mazishi ya Seneta Boy.