Gavana wa Kwale Salim Mvurya amewakosoa Gavana wa Mombasa Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi, kwa kile alichokitaja kama kuingilia masuala ya kaunti yake.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiwahutubia wakaazi katika eneo la Msambweni, Mvurya aliwataka magavana hao kukoma kuandaa mikutano katika Kaunti ya Kwale bila ya kumhusisha.

“Mnafanya mikutano katika kaunti zingine bila kumjulisha gavana mwenzenu. Si hiyo ni uchochezi? Ni mambo kama haya ambayo sisi hatutakubaliana nayo. Itakuaje viongozi wa Kilifi na Mombasa watafanya mikutano hapa Kwale bila kiongozi yeyote wa kaunti kujulishwa?” aliuliza Mvurya.

Haya yanajiri baada ya kuibuka madai kuwa Gavana Mvurya anasusia masuala ya chama cha ODM, kwa vile amekua kibaraka wa chama cha Jubilee.

Hata hivyo, Mvurya amesema kuwa hatababaishwa na wanaojaribu kumharibia jina kwa kumtaja kama kibaraka wa Jubilee.

Aidha, alisema kuwa hatosita kufanya kazi na serikali kuu, kwa manufaa ya wakaazi wa Kwale.