Mgombea mwenza wa kiti cha ugavana Kaunti ya Mombasa Anania Mwaboza katika hafla ya awali. Picha/ the-star.co.ke

Share news tips with us here at Hivisasa

Mgombea mwenza wa kiti cha ugavana Kaunti ya Mombasa Anania Mwaboza amesema kuwa licha ya serikali ya Kaunti ya Mombasa kupokea ushuru wa shilingi laki 900,000 kutoka kwa soko la Kongowea, bado soko hilo linakumbwa na changamoto nyingi za kimaendeleo.Akiongea mjini Mombasa, Mwaboza alisema ni wazi kuwa serikali ya kaunti inapokea fedha hizo lakini hakuna hatua zozote za kuboresha huduma sokoni humo.Mwaboza alihoji kuwa sharti serikali ya kaunti kuweka mikakati kabambe ya kuboresha viwango vya biashara katika soko hilo.Mwaboza ameitaka serikali ya kaunti kueleza jinsi imetumia fedha wafanyabiashara wanazotozwa kama ushuru.Wakati huo huo, Mwaboza ameiunga mkono kauli ya Rais Uhuru Kenyatta kuwa serikali ya Kaunti ya Mombasa imepokea kima cha shilingi bilioni 40 kutoka kwa serikali kuu.Mwaboza alisema kuwa imebainika wazi Kaunti ya Mombasa hadi kufikia sasa imepokea jumla ya shilingi billion 43.79.Mwanasiasa huyo alisema kuwa ni jukumu la serikali ya kaunti kuwafahamisha wakaazi jinsi fedha hizo zilivyotumika.Aidha, Mwaboza alielezea wasiwasi wake kwamba kuna fedha nyingi za ufadhili kutoka kwa nchi za kigeni ambazo bado haijabainika zilivyo tumika, hatua aliyoitaja kudhihirisha kuwa serikali ya kaunti inahusika katika ufujaji fedha za umma.