Chama tawala cha Jubilee kimevutia mgombea mpya wa ugavana Kaunti ya Mombasa baada ya aliyekuwa mbunge wa Kisauni Ananiah Mwaboza, kujitupa ulingoni.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwaboza, ambaye ni mshauri wa afisi ya naibu wa rais William Ruto ametangaza azma yake ya kugombea kiti cha ugavana Kaunti ya Mombasa katika uchaguzi wa 2017 kupitia tiketi ya chama cha Jubilee.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee, Mwaboza alisema kuwa ameamua kuwania kiti hicho kufuatia msukumo na wafuasi wake wa chama cha Jubilee, pamoja na wakaazi wa Mombasa, kwa lengo la kuyaleta maendeleo mashinani.

Huku hayo yakjiri, mwenyekiti wa Jubilee tawi la Mombasa Ali Mwatsahu amesema chama cha Jubilee kina umaarufu sana katika kaunti hiyo.

Wengine ambao wanatarajiwa kugombea wadhifa huo kwa tikiti ya Jubilee ni Suleiman Shabal, Hamis Babangida, Najib Balala na Abdalla Mwaruwa.

Muungano wa Jubilee unatarajiwa kutangaza rasmi kiongozi atakayepeperusha bendera ya muungano huo katika kiti cha ugavana wa Mombasa mwezi ujao, Rais Uhuru Kenyatta atakapozuru kaunti hiyo kufungua rasmi maonyesho ya kilimo Mombasa na soko la Kongowea.