Khamis Mwaguya, aliyekuwa katibu wa serikali ya Kaunti ya Mombasa, ameteuliwa kuwa mkuu wa idara ya biashara, nishati na uwekezaji.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwaguya aliteuliwa na bunge la kaunti ya Mombasa siku ya Jumatano.

Hii ni baada ya kufanyiwa ukaguzi na kamati maalum ya bunge hilo, wiki iliyopita, na kamati hiyo kuafiki kuwa Mwaguya alikuwa ametimiza masharti hitajika kupewa wadhfa huo.

Wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge la Mombasa Khamis Mwidani, kamati hilo lilisema kuwa Mwaguya amekuwa mchapa kaz,i huku wakitoa changamoto kwa vijana kuiga mfano huo.

Mwaguya alihudumu kama katibu wa serikali ya Kaunti ya Mombasa kabla Gavana Hassan Joho kufanya mabadiliko mapema mwezi Februari mwaka huu, na kumchagua kuwa mkuu wa wafanyikazi.