Mbunge wa Likoni Masoud Mwahima ameikashifu bunge la kaunti ya Mombasa kwa kupitisha mswada wa kuiruhusu serikali ya kaunti hiyo kununua shamba la Waitiki akisema kuwa serikali ya kaunti hiyo imeingiza siasa katika jambo hilo.
Mwahima ambaye alikuwa akihutubia wananchi katika eneo la Shika adabu siku ya Jumatatu alisema kuwa iwapo serikali kuu ilikuwa imekubali jinsi malipo ilivyotakikana kufanywa basi si vyema serikali ya kaunti kuingilia ikijidai ilikuwa ikiwasaidia wakaazi hao.
Mwahima amesema kuwa Gavana Joho huenda anatafuta umaarufu wa kisiasa kupitia kwa maadai kuwa serikali ya kaunti itanunua shamba la Waitiki kwa niaba ya wakaazi.
Mwahima sasa anaitaka serikali kuu kuendesha mambo ya ardhi hiyo kama vile walivyokubaliana hapo awali bila ya kizuizi kutoka kwa serikali ya kaunti.