Mbunge wa Likoni amewataka magavana wa kanda ya Pwani waliobuni muungano wa jumuiya ya kaunti za Pwani kueleza manufaa ya muungano huo kwa mwananchi tangu kubuniwa kwake.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza na waandishi wa habari, Masoud mwahima alisema kwamba muungano huo unaonekana kutokua na manufaa yoyote kutokana na mzozo baina ya magavana huo.

Mwahima alisema kuwa baadhi ya magavana wamegundua ufisadi uliopo katika muungao huo, jambo liliowafanya kujiunga na serikali ili kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo katika maeneo wanayowakilisha.

Mwahima alisema tangu vurugu kushuhudiwa kwenye muungano huo, hakujatolewa njia mwafaka zinazoonyesha namna muungano huo ulivyotimiza ahadi zake, ama unavyoafikia malengo yake.

Mbunge huyo alisema kuwa kutatua tatizo la uhaba wa maji ilikuwa mojawapo ya malengo la muungano huo ila hilo halijaafikiwa kufikia sasa.

“Hakuna la kuficha wala la siri. Ukweli ni kwamba hata baadhi ya magavana wametambua kuwa mrengo wa upinzani ulihusika pakubwa katika kubuni muungano huo, jambo ambalo liliyeyusha maazimio ya magavana kwa wananchi waliowachagua. Leo hii tukiungana na Jubilee bado wanaongea lakini hili hawalioni,” alisema Mwahima.

Hata hivyo, amesema kuwa wakati wa Wapwani kujitambua umefika, huku akiongeza kuwa wakaazi wanapaswa kushirikiana na serikali ili waweze kunufaika na miradi ya maendeleo.

Mwahima ni kati ya viongozi kutoka Pwani walioasi chama cha ODM na kujiunga na Jubilee.