Hatimaye mbunge wa Likoni Masoudi Mwahima ametangaza rasmi kuhama muungano wa CORD na kujiunga rasmi na muungano wa JAP.
Akizungumza huko Likoni Jumatano, Mwahima amesema ameafikia uamuzi huo kama njia ya kurejesha shukrani kwa Rais Uhuru Kenyatta kutatatua mzozo wa shamba la Waitiki.
Mwahima ambaye ni mbunge wa ODM alikutana hivi majuzi na Rais katika ikulu ya Mombasa na tetesi zikazagaa kuhusu picha yake akitoka ikulu hiyo akiwa amebeba bahasha.