Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwakilishi wa wadi ya Sengera Bosoti, eneo bunge la Bomachoge Chache Timothy Nyarang’o, amemuomba mbunge wa eneo hilo Simon Ogari, kuingilia kati na kufuatilia kilichosababisha ukarabati wa barabara ya Omoringamu-Sengera kukomeshwa.

Hii ni baada barabara hiyo kuorodheshwa miongoni mwa barabara zitakazokarabatiwa na shirika laa ‘Kenya Rural Roads Authority' (KeRRA) na baadaye kusemekana hakuna pesa za kukarabati barabara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano katika wadi yake, mwakilishi huyo alisema hajafurahishwa na hatua hiyo na kuomba mbunge Ogari kuingilia kati kubaini chanzo cha kutokarabatiwa kwa barabara hiyo.

“Naomba mbunge wa eneo bunge hili Simon Ogari kuuliza kwa nini ukarabati wa barabara ya Omoringamu-Sengera ulikomeshwa baada ya kusemekana hapo mbeleni kuwa itakarabatiwa,” alisema Nyarang’o.

Aliongeza “Pesa zile barabara hiyo ilitengewa hapo awali zilienda wapi? Naomba mbunge wetu aulize ili tupate jibu halisi.”

Nyarang’o alisema kuwa barabara hiyo ambayo imesusiwa kukarabatiwa hutumika kuunganisha soko la Sengera, shule ya msingi ya Sengera, na shule ya Nyabioto hadi eneo la Riokindo.