Mwakilishi wa Wadi ya Magenche iliyoko eneo Bunge la Bomachoge Borabu, Kaunti ya Kisii Timothy Ogugu ametishia kurudisha pesa za maendeleo za Wadi yake kwa Serikali ya Kaunti baada ya mwanakandarasi aliyepewa kandarasi ya kujenga zahanati ya Kiabugesi kinyume na makubaliano ya awali.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Jumatano jioni katika eneo la Eberege, mwakilishi huyoaliwaonya wanakandarasi wote katika Wadi hiyo ambao hawafanyi kazi kama inavyostahili kuwa watachukuliwa hatua ya kisheria kwani pesa zinazotumika ni za mkenya wa kawaida kufanyiwa maendeleo.

“Mwanakandarasi yeyote hafanyi kazi kwa kiwango kile kinachostahiliwa atachukuliwa hatua ya kisheria maana pesa hizi mnapatiwa ni za maendeleo katika Kaunti hii ambazo hutoka kwa mwananchi baada ya kutozwa ushuru,” alisema Mwakilishi Ogugu.

Mwakilishi huyo alianzisha ujenzi wa zahanati sita katika Wadi yake hiyo jana kwa kutumia pesa hizo za maendeleo huku akiwaonya wanakandarasi kuwa wasipohitimu kama inavyohitajika, basi hawatapokezwa pesa ila kurudishwa kwa Serikali.

Miongoni mwa zahanati alizoanzisha ni Eberege, Nyabiore, Itembu, Riogachi na Magenche. Wakati uo huo Mwakilishi huyo alianzisha ujenzi wa madarasa ya ECD katika shule za msingi katika Wadi hiyo.