Mwakilishi wa wadi ya Magenche, eneo bunge la Bomachoge Borabu, kaunti ya Kisii amewaomba washikadau wote wa shule zilizoko kwa wadi yake kushirikiana ili kuinua viwango vya elimu katika eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Jumatatu katika mkutano uliokua katika shule ya upili ya Binyinyi ilioko kwa wadi yake, Timothy Ogugu, alisema kupitia ushirikiano viwango vya elimu vitapanda juu zaidi kuliko wakati hakuna ushirikiano.

Aidha, mwakilishi huyo aliwataka washikadau hao wa shule hiyo kuwa na motisha ya kuhakikisha wanafunzi wamepata elimu ambayo inahitajika ili wanafunzi wawe wanapita katika mitihani ya kitaifa.

“Ushirikiano mwema kati ya wazazi, walimu nami mwakilishi wenu utahakikisha viwango vya elimu vimekua vya vya hali ya juu katika wadi hii,” alisema Timothy Ogugu.

Aliongezea: “Nahitaji wadi yangu ifanye vyema kuliko wadi zingine zilizoko katika kaunti hii ili wanafunzi wafurahie matokeo mema baada ya matokeo ya mitihani kutangazwa.

Kwa upande mwingine washikadau hao waliahidi kuwa na ushirikiano kati yao na mwakilishi huyo ili kuinua viwango vya elimu katika eneo hilo huku wakimtaka mwakilishi huyo kutimiza yale amesema ili isiwe ni kusema na kunyamanza.

“Tunakuomba utimize yale uliyoyasema hapa leo. Sisi sote tunataka wanafunzi wapite mtihani. Tunakuomba utukumbuke wakati tutakapo hitaji misaada mbalimbali kama vile ya vitabu,” alisema Erick Mochama msimamizi wa shule hiyo ya Binyinyi.