Mwakilishi wa eneo la Bogichora Beautah Omanga amejitokeza kulalamikia hali mbovu ya barabara katika eneo lake na uwakilishi wake.
Akihutubu katika shule ya upili ya Sironga kwenye hafla ya mazungumzo ya pamoja yaliyo na dhana ya kujiandaa kwa siku ya kongamano la ugatuzi nchini kule Meru siku ya Alhamisi, Omanga alisema kuwa barabara za Nyamira-Mabundu, Na sironga-Makairo ziko katika hali mbaya na zinahitaji kurekebishwa.
"Ukweli ni kwamba barabara ya Nyamira-Mabundu na ile ya Sironga-Makairo ziko katika hali mbaya, na ni ombi langu kwa serikali kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo," alisema Omanga.
Omanga aidha alilalama kuwa eneo hilo limekuwa likitengwa kwa muda kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo, hali iliyomlazimu.kumtaka gavana Nyagarama kuwaachisha kazi mawaziri wasiowajibika kazini.
"Huu ni mwaka wa nne tangu serikali za ugatuzi zianzishwe, na ukweli ni kwamba eneo wadi hili halijanufaika kutokana na miradi ya maendeleo, na ndio maana namtaka gavana kuwaachisha kazi mawaziri wazembe kwa kuwa kuna watu waliohitimu kuchukua nafasi za kazi," aliongezea Omanga.