Mwakilishi wa wadi ya Gesima Kennedy Nyameino ameomba wakaazi kushirikiana ili kuinua viwango vya maendeleo katika eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea ijumaa katika hafla ya mazishi ya kijana wa mwenyekiti wa taasisi ya Enchoro, Peter Minyira, Nyameino alisema kuwa uhusiano mwema ni chanzo cha maendeleo.

“Niko tayari kushirikiana nanyi ili kuinua viwango vya maendeleo na nitahakikisha kuwa nimewaakilisha vyema katika bunge letu la Nyamira,” alisema Nyameino.

Aidha, aliongezea kuwa atafanya kila awezalo kuendeleza miradi ambayo itasaidia kuinua viwango vya maendeleo.

“Kama twataka kufurahia matunda ya ungatuzi lazima sisi sote kama wakaazi wa eneo hili tujiunge pamoja bila kujali koo zetu,” akadokeza Nyameino.

Wakati huohuo Nyameino aliahidi kuikarabati barabara ya kutoka Gesima kuelekea mahali ambapo kiwanda kipya cha majani chai kinajengwa.

“Hatua hii itarahisisha shughuli ya ujenzi wa kiwanda hicho,” alisema Nyameino.

Pia alisema kuwa ujenzi huo utakapomalizika utasaidia watu wengi hasa vijana ambao alisema watapata ajira.

Aliwaomba vijana kutozembea masomoni akisema kuwa masomo ni guzo muhimu.