Mwakilishi mteule kutoka wadi ya sengera bosoti kaunti ya Kisii Felstus Metobo amewaomba wananchi kutoandamana na kupanda migomba ya ndizi barabarani kulalamikia barabara mbovu ila kufuata mkondo ulio na suluhisho.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea na mwanahabari huyu siku ya Jumatatu, mwakilishi huyo alikiri kuwa wananchi sharti wasubiri na kuwapa viongozi wao mda kwa kufanya maendeleo, kwani ni miaka miwili tu viongonzi hao wamekuwa katika mamlaka na kuwasihi wananchi kutoandamana kamwe na kufuata njia ya kueleweka ili kupata suluhu halisi kuhusu wanalolalamikia.

Wakati huo huo, mwakilishi huyo aliwaomba viongonzi wote wa eneo lote la Kisii kujiunga pamoja na kuwafanyia wananchi maendeleo ambayo ni haki yao, kwani wananchi ndio huwachagua viongonzi.

“Nawaomba viongonzi wa eneo la Kisii tujiunge pamoja na wananchi washirikianane nasi kwa ujumla ili eneo letu lionekane kuwa la maendeleo katika nyakati zijazo,” alisema Metobo.

Aidha, mwakilishi huyo aliowaomba wananchi kutowakosoa viongonzi wao kwa kutofanya maendeleo dhidi yao kwa haraka, na kuwajulisha maendeleo yanafanywa kwa utaratibu na kiongozi hawezi tekeleza maendeleo wakati mmoja ila ni kufuata utaratibu na orodha ya kufanya maendeleo hayo katika sehemu mbalimbali husika

“Sisi kama viongonzi, tunaomba mtupe nafasi, tutatekeleza kila jambo la maendeleo kwenu, la muhimu ni kuwa na subira maana lazima tutimize yale viongonzi uwahidi,” aliongezea Metobo.

Mwakilishi huyo amewahakikishia wananchi kuwa watafanyiwa maendeleo kikamilifu kabla ya uchaguzi ujao.