Mwakilishi wa Wadi ya Bogiakumu ndani ya bunge la Kisii amelaumu usimamizi wa kaunti hiyo kwa kufanya miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa barabara kwa ubaguzi, hasa mipaka ya maeneo bunge.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza wakati alipoitembela barabara iliyoko katika eneo lake siku ya Jumaa, Richard Bundi, ambaye ni mwakilishi wa wadi hiyo alisema kuwa kulikuwa na makubaliano ya utengezi wa barabara ya Nyanchwa-Riamaranga wakati alipomtembeza Gavana wa Kaunti katika eneo lake, walakini hadi sasa hamna lolote ambalo limefanywa.

Bundi aidha alisema kwenye mpango huo wa makubaliano, barabara inayopakana na eneo bunge la Bonchari imewachwa, huku ile inayoshughulikia eneo bunge la Kitutu Chache imeundwa ikakamilika,

“Mbona kubagua maeneo ya kufanya maendeleo ilhali wote hawa ni watozwa ushuru ndani ya kaunti ya kisii, kwani wao hawahitaji barabara?” aliuliza mwakilishi huyo.

“Watu wangu ndio wauzaji wa miwa, ndizi na njugu katika kaunti ya kisii, ikakuwaje kwamba ndio wanosafiri mwendo mrefu, kutozwa ushuru na barabara hawatengezewi?” aliongezea mwakilishi huyo.

Kulingana naye, nyakati za mvua zinapoingia, huenda wanafunzi  na wazazi wakawa hawana lingine ila kutumia barabara mbadala iliyoko mbali kuepuka hatari ya majeraha ambayo huenda yakashuhudiwa kutokana na hali mbaya ya barabara hiyo.

“Nitalazimika kuwarai wananchi katika wadi yangu kutotoa ushuru ikiwa raslimali zao hazitambuliwi na utawala wa kaunti ya kisii vikamilifu”, alionya mwanasiasa huyo.