Mwakilishi wadi ya Sameta Bwa Siko Obwogi amethamini mafunzo bila malipo kwa wanabodaboda wa wadi yake, na kuahidi kuwanunulia vijana wengine pikipiki kutumia baada ya mafunzo hayo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwakilishi huyo, ambaye alishuhudia zoezi la vijana hao kupewa leseni kwa wale walikuwa wamefuzu katika uwanja wa shule ya wavulana ya Sameta aliwashukuru vijana ambao wamejitolea kushiriki katika mradi huo, na kuwaomba kuendelea kudumisha heshima na kufuata sheria za trafiki barabarani.

Pia, aliongeza kusema kuwa analenga kuweka pesa ya maendeleo ya wadi kuwapa vijana kama mkopo ili kuendeleza biashara na shughuli za kujiimarisha kiuchumi.

Bwa Obwogi aliwataka vijana kutoka wadi hiyo kuhakikisha kuwa wamejiandikisha katika makundi kama njia mojawapo ya kujiweka katika nafasi ya kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha kama mabenki na vyama vya mashirika.

“Nawaomba nyinyi mkiwa vijana mjiweke katika makundi na kuandikisha mapendekezo ya kupata mikopo kutoka kwa taasisi za fedha, hata mimi nitakuwa tayari kuwasaidia kupitia pesa za maendeleo ya wadi, kuwa wazi kutembelea ofisi yangu ili mpate ushauri jinsi ya kupata msaada,” mwakilishi huyo aliwaomba vijana.

Bwana Obwoge amekuwa mwakilishi wa kwanza kufadhili vijana hao wa bodaboda ambao waekuwa wakilaumiwa sana na wateja kuwa hawana mafunzo ya kwendesha pikipiki, ambapo kumeshuhudiwa ajali nyingi za barabarani.