Mwakilishi wa wadi ya Bogeka Charles Mochoge Nyagoto kutoka eneo bunge la Kitutu Chache Kusini Kaunti  ya Kisii ameipongeza serikali kuu kwa kupunguza kiwango cha kuunganishiwa stima kwa wakenya wote.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi huyo alikuwa akiongea katika uwanja wa Gusii kwenye hafla ya kusherehekea siku kuu ya Madaraka, alipogeza serikali kuu kwa kupunguza kiwango cha pesa kinachoitajika ili mtu kunganishiwa stima na kusema itasaidia pakubwa ili kila mwananchi wa kawaida aweze kufaidika

Kwa upande mwingine aliiomba serikali kuu kuweka mikakati kabambe kwa kuwa watu hulipa pesa nyingi kwa kila mti wanapowekewa stima na kuomba kuwa  iziwe ni kupunguza kuwekewa ‘Cable’ na kuiomba kuwa iwe walipunguza  kila kitu.

“Watu hulipa pesa nyingi wakati wa kuunganishiwa stima haswa kwa kila mti  unaostahili kufikisha stima kwa mwenye anaitaji kuwekewa,” alihoji Nyagoto.

Kulingana na mwakilishi Nyagoto alisema kuwa kiwango cha mti huwa zaidi ya shillingi elfu 15 na kama mtu anatakiwa  miti tatui ili  kupate stima huwa ni elfu 45 na ukiongeza  za kuunganisha shillingi elfu 15 pesa hizo huwa ni zaidi i kwa mwanaichi wa kawaida.

Kwa sasa ameiomba serikali kuu kushirikiana na sekta  ya Nguvu  za Umeme kuwaeleza wakenya kama pesa hizo ni za shughuli nzima au ni za kuunganisha na za  mti ziko kando.