Mwakilishi wa wadi ya Bogeka Charles Mochoge Nyagoto kutoka eneo bunge la Kitutu Chache Kusini Kaunti ya Kisii ameipongeza serikali kuu kwa kupunguza kiwango cha kuunganishiwa stima kwa wakenya wote.
Mwakilishi huyo alikuwa akiongea katika uwanja wa Gusii kwenye hafla ya kusherehekea siku kuu ya Madaraka, alipogeza serikali kuu kwa kupunguza kiwango cha pesa kinachoitajika ili mtu kunganishiwa stima na kusema itasaidia pakubwa ili kila mwananchi wa kawaida aweze kufaidika
Kwa upande mwingine aliiomba serikali kuu kuweka mikakati kabambe kwa kuwa watu hulipa pesa nyingi kwa kila mti wanapowekewa stima na kuomba kuwa iziwe ni kupunguza kuwekewa ‘Cable’ na kuiomba kuwa iwe walipunguza kila kitu.
“Watu hulipa pesa nyingi wakati wa kuunganishiwa stima haswa kwa kila mti unaostahili kufikisha stima kwa mwenye anaitaji kuwekewa,” alihoji Nyagoto.
Kulingana na mwakilishi Nyagoto alisema kuwa kiwango cha mti huwa zaidi ya shillingi elfu 15 na kama mtu anatakiwa miti tatui ili kupate stima huwa ni elfu 45 na ukiongeza za kuunganisha shillingi elfu 15 pesa hizo huwa ni zaidi i kwa mwanaichi wa kawaida.
Kwa sasa ameiomba serikali kuu kushirikiana na sekta ya Nguvu za Umeme kuwaeleza wakenya kama pesa hizo ni za shughuli nzima au ni za kuunganisha na za mti ziko kando.